Barabara yakatika eneo la Mtondia huko Kaunti ya Kilifi kufuatia mvua Kali inayoendelea kunyesha huko pwani. Maji yanazidi kutiririka kutoka eneo la Kilifi lililo juu yakielekea Malindi na kusababisha usafiri kusambaratika. Wale ambao wanasafiri ima kutoka Kilifi kuelekea Malindi ama Malindi kuelekea Kilifi na Mombasa kwa ujumla wanaombwa wawe makini barabarani. Sehemu salama ya kupitia ni Bofa.
Kaunti ya Kilifi ikishirikina na wizara ya usafiri inaombwa mara moja kushughulikia hali hii ili kurudisha huduma za usafiri katika hali nzuri. Tazama video hii kwa habari zaidi.