Mchungaji wa kanisa la Good News International Church Paul Mackenzie amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela bila faini. Mackenzie amehukumiwa kwa mashtaka kadhaa yakiwemo kupeperusha mahubiri na filamu bila leseni halali, kumiliki studio ya filamu bila leseni.
Akitoa hukumu hiyo hakimu Oga Onalo wa mahakama ya Malindi amezingatia vigezo kadhaa vikiwemo; umri wa Mackenzie na kanisa alilokuwa akihudumu lilikuwa limefungwa tayari.Mackenzie amejipata na mashtaka yanayohusiana na vifo vya watu mia nne ishirini na tisa (429) ambao miili yao tayari imefukuliwa katika vichaka vya Shakahola. Mackenzie pia amehusishwa na mafunzo ya itikadi kali yanayopotosha watoto kama vile kuacha shule, kuchoma vitabu na kwenda kanisani kwake. Mackenzie atahukumia kifungo chale katima magereza ya Shimo la Tewa.