Home Swahili TALANTA SI NDUMBA! MFAHAMU MWANDISHI MCHANGA ALIYEANDIKA NA KUCHAPISHA MATOPA YA VITABU!

TALANTA SI NDUMBA! MFAHAMU MWANDISHI MCHANGA ALIYEANDIKA NA KUCHAPISHA MATOPA YA VITABU!

by Kaka Benayah

Kelvin Kipkoech, anayejulikana kama Salim, ni mwandishi mchanga na mwenye nia, malengo na talanta ya uandishi. Ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini kwa sasa na ambaye anatoka katika Kijiji cha Kipsomor huko Chebangang, Wadi ya Kimulot, Eneobunge la Konoin, Kaunti ya Bomet, Mkoa wa Bonde la Ufa Kusini.Mwana mpendwa wa Bw na Bi Ruto, wazazi ambao huwahifadhi watoto wao kwenye kipande kidogo cha ardhi bila kazi rasmi na kuishi tu kwa kijungu jiko alimuradi mkono uende kinywani.

IMG 20240327 WA00131
Kelvin Salim akiwa na vitabu vyake

Kipkoech, kama watoto wengine, alisomea moja ya shule za msingi katika Wadi ya Kimulot na kufaulu KCPE yake kwa kishindo, alama zilizomwezesha kupata nafasi katika shule ya kutwa ya Chebang’ang eneo bunge la Konoin, ambapo alitia makali ujuzi wake wa kuandika. Alishinda zawadi nyingi ndani na nje ya shule.Alipokuwa kidato cha pili, akiwa na umri wa miaka 15 haswa, aliandika kitabu chake cha kwanza, THE DIM STAR. Licha ya kukumbatiwa na wanafunzi wenzake na walimu, kilikuwa kimemfanya apitie motoni mikononi mwa mchapishaji.

Alipokuwa akitafuta sana njia za kuchapisha kitabu chake cha kwanza, alikutana na Mkurugenzi Mtendaji (jina linahifadhiwa) ambaye alijitolea kuchapisha kitabu chake kwa kiasi kilichokubaliwa.Kipkoech haraka alikimbilia kwa wazazi wake, ambao tayari walikuwa wamefilisika, na kuwasilisha kesi yake kwao.Kama Waswahili wasemavyo: Ng’ombe akivunjika guu malishoni, hukimbilia zizini, ndivyo mwandishi alivyofanya.Baba yake alishindwa kuongea neno lolote lile, bali aliendelea kumkodolea macho mwanae huku akiwaza ni kitu gani afanye ili kumsaidia kufikia lengo lake la kuwa mwandishi maarufu.Baada ya kumtazama mwanae kwa muda machozi yakimtiririka, alinyanyuka kwenye kiti chake na kutoka nje. Mama naye alitokwa na machozi, akamfuata mume wake kipenzi nje na wote wawili wakatazama mawingu kwa huzuni na kuomba Mola awakumbuke.

Wakati uo huo, mama yake alimpa simu yake mwandishi mchanga na mwenye matumaini ili kuiweka kwa mauzo, ambayo Kipkoech aliikaribisha kwa kusitasita.Baada ya siku mbili, Kipkoech alimwendea mchapishaji wake ambaye alikuwa amejitolea kuchapisha kazi yake, bila kujua kwamba Mkurugenzi Mtendaji huyo alikuwa mbwa mwitu chini ya ngozi ya kondoo.Mkurugenzi Mtendaji alichukua pesa alizopokea kwa kuuza simu pekee ya mama masikini na kutokomea hewani. Hadi leo, Kipkoech anamwomba mtu huyo asiye na utu amrejeshee hela.Kipkoech aliporudi nyumbani na kutoa habari mbaya kwa wazazi wake, nyumba hiyo ikawa nyumba ya vilio hadi siku iliyofuata.Licha ya changamoto ambazo Kipkoech alikabiliana nazo katika kuelekea kuwa mwandishi mashuhuri, aliweza kuchapisha riwaya yake ya kwanza, ya pili na ya tatu kutokana na usaidizi wa watu waliomtakia mema na wazazi wake maskini.

Mbali na kitabu chake cha kwanza cha THE DIM STAR, Kelvin pia amechapisha NILICHOSHIDWA KUTIMIZA, LURING WHISPERS OF LOVE, MEMORIES OF NINA na NITAMUUA SHEMEJI.Kelvin anamshukuru sana Bwana Pascal Null Watua ambaye alikuja katika maisha yake na kubadilisha huzuni yake kuwa furaha kwa kuhariri kazi yake na kumtia moyo kila siku.NILICHOSHIDWA KUTIMIZA ni juhudi za pamoja za Kipkoech Kelvin na Eva Mrema Smile kutoka Tanzania.NITAMUUA SHEMEJI ni riwaya nyingine tamu ya upelelezi ya Kelvin Kipkoech Salim na Bi. Sumaiyah Binti Swalleh, mwalimu wa shule ya upili.LURING WHISPERS OF LOVE ni riwaya ya Kiingereza ambayo aliuza sana licha ya kutokuwa na hela nyingi za uchapishaji.

Baada ya kufanya utafiti kwa muda aliandika wasifu wa Rais Ruto na kuupa jina la MTUKUFU RAIS.Tangu atoke kwenye lango la shule miaka michache iliyopita, Kelvin Kipkoech amekuwa mwandishi kamili, akitumaini kwamba siku moja Mungu atamtuma msaidizi wa kumshika mkono na yawe maombi yake kwamba siku moja mtoto wa mkulima apate chakula cha jioni pamoja na mfalme katika jumba lake la kifalme.Wasiliana na mwandishi kwa nambari yake ya simu; 0718156161

You may also like

Leave a Comment

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?