Home articles Historia fupi ya Mwanzo na mwisho wa KCPE nchini Kenya

Historia fupi ya Mwanzo na mwisho wa KCPE nchini Kenya

by Kaka Benayah

Ama kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tangu mwaka wa elfu kenda mia themanini na tano(1985), mtihani wa KCPE ulianza kufanya kazi katika Elimu nchini Kenya. Sasa, ni takriban miaka thelathini na minane( 38) ikiwa bado imeshika kasi. Wengi wakipitia mfumo wa Elimu wa 8-4-4 ya KCPE kufanya mtihani wao wa shule ya msingi na upili.

Leo hii imefika kikomo. Mwisho wake hasa mwaka huu wa 2023. Licha ya siku hii kuandikwa na hata kuwa siku ambayo itakumbukwa na wengi, pia ni siku bab’kubwa kwa watahiniwa waliofanya mitihani yao ya Kitaifa namatokeo kutangazwa. Hongera kwao! Wanafunzi hao waliofanya mitihani walifanya vyema huku mwanafunzi kwa jina; Michael Warutere (Shule ya msingi ya Riara springs Academy)aliyeibuka kifuambele akiwa na alama 428 , Jacinta Bethany Khasundi (Shule ya msingi ya St. Anne’s Mumias) akiwa na 427 kisha Khadija Yunis (Shule ya Msingi ya Light Academy Mombasa) 426.Wanafunzi hao wamesherehekewa kwa kufanya vyema katika mtihani huo na hata kuelezea furaha yao kwa ajili ya matokeo hayo.

( Mwandishi, Alfred Lobawoi). Alfred ni mwanahabari mwandishi mwenye tajiriba kubwa katika uandishi wa makala tofauti.

You may also like

Leave a Comment

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?