Saturday, December 21, 2024
Saturday, December 21, 2024
Home sports GUNDU LAMWANDAMA REECE JAMES!

GUNDU LAMWANDAMA REECE JAMES!

by Kaka Benayah

Kuangukako ndiko kuinamako. Hii ni methali mashuhuri ya waswahili inayonuiwa kuwatia moyo wanadamu. Hususan katika wakati wa matatizo na changamoto. Hii ni kinyume kabisa kwa Nahodha wa Chelsea Reece James. Awali kabla ya michuano ya kimataifa, James alihusishwa katika mchuano wa dabi didhi ya Arsenal akiingia kama mchezaji wa akiba katika mtanange ulioishia kwa sare ya kufungana goli moja.

Leo tena masaibu bado yanamwandama na kumvizia James. Nahodha huyo amepata jeraha jipya la goti. Jeraha hilo huenda likamweka mkekani kwa zaidi ya mwezi mmoja. Hii sio mara ya kwanza majeraha kumwandama mlinzi kisiki huyo wa Wanasamawati wa “The Blues”. Uwezo na maarifa aliyonayo James angewafaa Chelsea hususan katika msimu huu. Msimu ambao Chelsea wanatia inadi na kuonyesha matumaini ya kunyang’anyira kombe kubwa la EPL.

Nahodha huyo ameandika waraka kwa Chelsea na Mashabiki wa Chelsea kwa jumla, akiwamiminia sifa na shukrani kede kede kwa kusimama naye kwa Kila aina ya njia nzuri hususan katika kipindi hiki kigumu cha taaluma yake. James pia amewarai mashabiki zake kuzidisha upendo katika msimu huu wa sherehe.

Nahodha huyo pia amewapa tumaini mashabiki na kuwaahidi kuwa hata kata tamaa katika wakati huu mgumu na atarudi kwa nguvu mpya, ari mpya na azma mpya. Sisi kama wapenzi wa kandanda tunazidi kumwombea James Kila la Kheri.

You may also like

Leave a Comment

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?