Saturday, December 21, 2024
Saturday, December 21, 2024
Home sports Kipute cha Ligi Kuu Nchini Uingereza Kimerudi Tena!

Kipute cha Ligi Kuu Nchini Uingereza Kimerudi Tena!

by Kaka Benayah

Papo kwa papo kamba hukat jiwe. Baada ya mapumziko mafupi ya wiki moja kwa ajili ya mechi za kimataifa, Ligi kuu Uingereza (EPL) imerudi tena. Imerudi kwa moto wa pasi kwani mitanange bab’kubwa inatarajiwa kusakatwa wikendi hii. Nyasi zitachanika sana leo hii kukiratibiwa kugaragazwa takribani mechi saba katika nyuga mbalimbali. Aisee kazi ipo leo. Msururu wa mechi za Leo huu hapa;

  • Manchester City Vs Liverpool- 3:30 pm
  • Newcastle Vs Chelsea- 6:00 pm
  • Burnley Vs West Ham
  • Shff United Vs Bournemouth
  • Nottingham Forest Vs Brighton
  • Luton Vs Crystal Palace
  • Brentford Vs Arsenal- 8:30 pm

Katika mitanange yote, akili macho na masikio yatajikita sana katika mchezo wa Man City wakichuana na watani wao wa jadi Liverpool katika uga wa Anfield. Man City wanatarajia kurudi tena katika njia ya kushinda baada ya kukabwa sare ya magoli manne na Wanasamawati wa Chelsea ugani the Stanford Bridge.

1700859868668
Mohammed Salah na Cody Gakpo wa Liverpool wakiwa mazoezini

Katika mtanange uliopita, Liverpool walimburuza Mwana Brentford mabao matatu bila jibu na wanapania kuipiku Man City iwapo watapat ushindi katika mtanange huo. Kupatikana kwa mchekaji na nyavu asiyeogopa kufunga mabao Erling Haaland kunaipa afueni Man City baada ya kutolewa kwa jeraha akiitumikia timu yake ya taifa Norway mapema wiki Jana. Watani hao ambao wamekuwa tishio katika ligi ya EPL wanaifanya mechi hiyo kuwa kubwa. Iwapo itaishia sare na Washika bunduki wa Arsenal wakapata ushindi ugenini Brenford, basi watakwea katika kilele cha Ligi hiyo na kukaa huko kwa furaha.

Arsenal na Brentford pia ni mchezo utakaotazamwa na wengi hususan baada ya kuwa na upinzani mkali baina ya timu hizi mbili. Miaka miwili iliyopita, Arsenal alibandikwa mabao mawili bila jibu na Wananyuki hao wa Brentford. Chelsea didhi ya Newcastle itarajiwa kuwa mechi ngumu vilevile huku Chelsea akijivunia fomu nzuri hususan baada ya kumkaba sare mwana Man City katika mtanange uliopita. Newcastle, ikijivunia kuwa klabu pekee iliyoifunga Arsenal msimu huu pia inatarajia kuendeleza fomu yao nzuri kwa ajili ya kutetea nne Bora.

Jumapili itashuhudia Mashetani wekundu wa Manchester United wakitoona kijasho na Everton ugani Goodison Park. Kurudi kwa mlinzli Luke Shaw kunatarajiwa kuipa nguvu Man United na kuendeleza fomu yao nzuri baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao moja didhi ya Luton katika mchezo wao wa mwisho.

You may also like

Leave a Comment

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?