Saturday, December 21, 2024
Saturday, December 21, 2024
Home Education MBUNGE WA KILIFI NORTH DAKTARI OWEN BAYA AIKABIDHI JAMII SHULE

MBUNGE WA KILIFI NORTH DAKTARI OWEN BAYA AIKABIDHI JAMII SHULE

by Kaka Benayah

Leo Tareehe 30 Januari ilikuwa siku kuu kwa wakaazi wa Magangani na Gede kwa ujumla. Mheshimiwa mbunge wa eneobunge la Kilifi Kaskazini leo hii ameikabidhi shule ya Gede Mixed Secondary School kwa jamii ya Magangani. Hii itakuwa hatua nzuri zaidi kwa wakaazi wa Magangani, Gede, Watamu, Kilifi na Kenya kwa ujumla kwani wanafunzi katika janibu zote wataipata elimu ambayo ndiyo ufunguo wa maisha.

1706637036698
Shule mpya ya Gede Mixed Secondary

Owen Baya, akizungumza katika mkutano wa kuikabidhi shule hiyo ameweka wazi yafuatayo.

1.Shule ya Gede Mixed imechukua takribani miezi kumi kukamilika. Hii inaonyesha ari na azma ya Mbunge Owen Baya katika jitihadi zake za kukamilisha miradi yake kwa wakati ufaao

2.Leo hii wanafunzi takribani 150 wamesajiliwa na kupokezwa kitita cha takribani Milioni Moja na nusu kwa ajili ya wanafunzi hao. Hii itakuwa nafasi adimu zaidi kwa wanafunzi waliomaliza darasa la nane 2023 na wanakumbwa na changamoto ya karo ili kujisajili katika shule za upili.

  1. Mheshimiwa mbunge pia amesisitiza kwamba Jumatatu ijayo ya tarehe 5 Februari masomo yataanza rasmi katika shule mpya ya Gede Mixed Secondary School.

4.Wanafunzi ambao wamesajiliwa na hawana sare za kuanzia katika shule hiyo ya msingi wamepewa nafasi ya kuanza masomo wakiwa katika sare za shule za msingi walikomalizia.

Idadi ya wanafunzi waliojiandikisha katika kidato Cha kwanza ni wanafunzi tisini na wanne huku idadi ya wanafunzi waliosajiliwa katika kidato cha pili ni wanafunzi ishirini na wawili. Mheshimiwa mbunge pia ameahidi kujenga maabara mpya katika shule hiyo muda wowote kutoka Sasa.

1706637556856
Mbunge wa Kilifi Kaskazini Daktari Owen Baya

Elimu ndio uti wa mgongo wa maisha. Elimu ni akiba na akiba haiozi. Ikioza hainuki na kama itanuka, basi haichefushi. Kwa niaba ya wakaazi wote wa Magangani, Gede na Kilifi kwa jumla, tunamwombea Mheshimiwa Mbunge kwa Mola ambariki na kumlinda anapoendelea kupigania elimu katika kaunti ya Kilifi

You may also like

Leave a Comment

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?