Washikabunduki wa Arsenal wamefanikiwa kushika namba mbili katika kinyang’anyiro cha ligi kuu nchini Uingereza mara tatu mtawalia. Baada ya kurithi mikoba kutoka kwa Arsene Wenger kuinoa Arsenal mkufunzi wa Arsenal amejitahidi si haba.
Kuirudisha Arsenal katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya si jambo dogo. Arsenal wamefanya hivyo kwa kishindo huku wakimtandika bingwa aliyeshinda makombe mengi ya UCL Real Madrid kipigo Cha mbwa msikitini.Hata hivyo Arsenal wameshindwa kwenda hadi kileleni na kuutwaa ubingwa wowote kwa kitambo kirefu hivi sasa. Funununu ambazo ni kisawe cha ukweli zinasema Arsenal wameshindwa kufanya hivyo kutokana na majeraha ya hapa na pale ambayo wachezaji muhimu kama Bukayo Saka, Gabriel Jesus na Kai Havertz wameyapata katika msimu huu.

Kilio cha Mashabiki cha kumrai kocha Arteta kusajili mshambuliaji kimehanikiza. Wachambuzi wa soka na wachezaji wa zamani wamedai kuwa mshambuliaji hatari ndicho kiuongo pekee kilichobaki ili kuiwezesha Arsenal kutwaa ubingwa na kubeba Mataji kadha wa kadha. Mshambuliaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokores Sasa ndilo jembe linalowindwa kwa udi na uvumba na washikabunduki hao wa Arsenal. Duru zinaarifu kuwa Viktor ambaye amekuwa akizitesa nyavu za timu pinzani yuko kwenye rada ya Arsenal na anatarajiwa kujiunga na Arsenal kwa mkataba wa miaka mitano baada ya Arsenal kukubaliana dau la Yuro Milioni 63 pamwe na nyongeza ya takribani Yuro Milioni 10 ili kuinasa saini ya mbabe huyo.
Arsenal hivi sasa Iko nchini Uhispaniola katika kambi ya La Manga walikokita kwa ajili ya mazoezi ili kujitayarisha kwa ajili ya msimu mpya utakaoanza baadaye mwezi wa nane mwaka huu. Viktor Gyokores anatazamiwa kukamilisha vipimo vya matibabu na kusafiri pamoja na wachezaji wenza kwenda nchini Singapore kwa ajili ya matayarisho zaidi.
Katika msimu huu wa 2024/2025 Gyokores amekuwa mwiba. Amefunga mabao sitini na matatu huku akichangia mengine kumi na Saba na kukamilisha jumla ya mabao themanini aliyochangia ima kwa kufunga au kutoa pasi zilizozalisha mabao. Mwamba huyu amefanya hivyo katika katika mechi hamsini pekee. Ni dhahiri atawasaidia wana Arsenal ikiwa watafanikiwa kuinasa saini yake pale Ugani Emirates
2 comments
Mko sawaaa lakin naona Chelsea ikiwa sawaaa zaidi
Good work n nice work